Show simple item record

dc.contributor.authorMWASAFU, HENRY MWALUGHA
dc.date.accessioned2019-05-15T09:51:06Z
dc.date.available2019-05-15T09:51:06Z
dc.date.issued2018-09-28
dc.identifier.urihttp://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/785
dc.descriptionUtafiti huu ulihusu uchunguzi wa maudhui na fani katika Utenzi wa Mwanamanga. Utafiti huu ulilenga kuchunguza maudhui na vipengee vya fani vilivyodhihirika katika utenzi huo. Utafiti huu vilevile ulilenga kubainisha hisia ambazo mtunzi amezitumia katika utenzi huo kwa kuangazia tamathali mbalimbali za usemi zilizotumiwa kuibua hisia hizo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kihemenitiki iliyoasisiwa na Friedrich Schleiermacher, Wilhelm Dilthey na Martin Heidegger. Msingi wa mtazamo wa kihemenitiki ni uchunguzi wa matendo mbalimbali ya binadamu kama usemaji, upendaji na uchukiaji. Nadharia hii inalenga kuchunguza mawasiliano pamoja na ufasiri wa maana za matini mbalimbali kama vile: kazi za kifasihi, vifungu vya Bibilia na vya kifalsafa. Utafiti huu ni wa kimaelezo ambapo umehusisha usomaji wa maktabani na vilevile kuzuru nyanjani. Katika usomi wa maktabani, makala, vitabu pamwe na tasnifu mbalimbali za fasihi zilisomwa ili kupata data iliyohusiana na utafiti huu. Utafiti huu kwa kiwango fulani ulihusisha usakuraji na ukusanyaji wa makala faafu kupitia kwa mtandao katika tovuti mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Katika utafiti wa nyanjani, mtafiti alifanya uteuzi wa kimakusudi ili kupata sampuli ya walengwa alionuia kupata data kutoka kwao. Utenzi wa Mwanamanga umedhihirisha maudhui ambayo baadhi yanahusiana na wanawake kama vile: urembo, unyumba, sifa, nafasi ya mwanamke katika jamii nakadhalika. Utenzi wa Mwanamanga umesheheni vipengee vingi vya fani ambavyo baadhi yavyo ni: tamathali za usemi kama vile: sitiari au mafumbo, taswira, tashbihi, ukiushi katika ushairi na muundo. Mtunzi wa Utenzi wa Mwanamanga ametumia hisia kama vile: kuona, kuonja, kunusa, kugusa na kusikia katika kumwelezea mhusika wake kwenye utenzi.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu uchunguzi wa maudhui na fani katika Utenzi wa Mwanamanga. Utafiti huu ulilenga kuchunguza maudhui na vipengee vya fani vilivyodhihirika katika utenzi huo. Utafiti huu vilevile ulilenga kubainisha hisia ambazo mtunzi amezitumia katika utenzi huo kwa kuangazia tamathali mbalimbali za usemi zilizotumiwa kuibua hisia hizo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kihemenitiki iliyoasisiwa na Friedrich Schleiermacher, Wilhelm Dilthey na Martin Heidegger. Msingi wa mtazamo wa kihemenitiki ni uchunguzi wa matendo mbalimbali ya binadamu kama usemaji, upendaji na uchukiaji. Nadharia hii inalenga kuchunguza mawasiliano pamoja na ufasiri wa maana za matini mbalimbali kama vile: kazi za kifasihi, vifungu vya Bibilia na vya kifalsafa. Utafiti huu ni wa kimaelezo ambapo umehusisha usomaji wa maktabani na vilevile kuzuru nyanjani. Katika usomi wa maktabani, makala, vitabu pamwe na tasnifu mbalimbali za fasihi zilisomwa ili kupata data iliyohusiana na utafiti huu. Utafiti huu kwa kiwango fulani ulihusisha usakuraji na ukusanyaji wa makala faafu kupitia kwa mtandao katika tovuti mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Katika utafiti wa nyanjani, mtafiti alifanya uteuzi wa kimakusudi ili kupata sampuli ya walengwa alionuia kupata data kutoka kwao. Utenzi wa Mwanamanga umedhihirisha maudhui ambayo baadhi yanahusiana na wanawake kama vile: urembo, unyumba, sifa, nafasi ya mwanamke katika jamii nakadhalika. Utenzi wa Mwanamanga umesheheni vipengee vingi vya fani ambavyo baadhi yavyo ni: tamathali za usemi kama vile: sitiari au mafumbo, taswira, tashbihi, ukiushi katika ushairi na muundo. Mtunzi wa Utenzi wa Mwanamanga ametumia hisia kama vile: kuona, kuonja, kunusa, kugusa na kusikia katika kumwelezea mhusika wake kwenye utenzi.en_US
dc.description.sponsorshipPwani Universityen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherPwani Universityen_US
dc.subjectMAUDHUI NA FANIen_US
dc.subjectUTENZI WA MWANAMANGAen_US
dc.subjectFUMO LIYONGOen_US
dc.titleUHAKIKI WA MAUDHUI NA FANI KATIKA UTENZI WA MWANAMANGA UTUNZI WAKE FUMO LIYONGOen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record