MATUMIZI YA MAFUMBO KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA SITI BINTI
Abstract
SHUKRANI
Naungama kuwa utafiti huu usingefaulu bila uwezo wa Mwenyezi Mungu. Mola ndiye
aliyewezesha safari hii kukamilika. Nilihitaji nguvu, uvumilivu, afya, hekima na hata
usalama na maelewano ili kuweza kufaulu. Haya yote yaliwezeshwa na mwenyezi
Mungu. Hali kadhalika nawashukuru walimu na wasimamizi wangu Prof. Rocha
Chimerah na Prof. Yakobo Mutiti kwa kujitolea mhanga kuhakikisha kuwa nimevuka hadi
kiwango kingine cha elimu. Mlinipa ushauri mwafaka ulionielekeza vizuri katika safari
hii ya uzamifu.
Shukrani za pekee nazielekeza kwa familia yangu kunga ikiongozwa na baba yangu
George Oloo na mama Rose Andeso kwa kupanda na kuotesha mbegu ya elimu ndani ya
maisha yangu. Mungu awape maisha marefu yenye amani katika dunia hii. Shukrani pia
kwa ndugu zangu Nancy, Mercy, Mourice na Martha ambao wamestahamili mengi ili
niweze kukamilisha safari hii. Mara nyingi nimekosa kuwaauni kwa hili na lile sababu
ikiwa kujilipia karo ya elimu ya juu, asanteni. Mwisho ningependa kumshukuru nyanya
yangu Eremina Oloo kwa ushauri ulionipa kuhusu maisha ya usomi. Ulinipa ushauri
mwafaka ulionipa msisimko wa usomi