• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UCHANGANUZI WA MAKOSA YA KIMOFOFONOLOJIA YA WANAFUNZI WA KIWAAṰA WANAPOJIFUNZA LUGHA YA KISWAHILI

    Thumbnail
    View/Open
    OMAR NAFISA AWADH.pdf (1.202Mb)
    Date
    2022-03-14
    Author
    AWADH, OMAR NAFISA
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utafiti huu ulihusu uchanganuzi wa makosa ya kimofofonolojia ya wanafunzi wa Kiwaaṱa wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Hivyo basi utafiti huu ulilenga kueleza Fonolojia ya lugha ya Kiwaaṱa kwa kufafanua sifa za irabu, konsonanti na arudhi yake, kubainisha na kuchanganua makosa ya kimofofonolojia yanayojitokeza miongoni mwa wanafunzi wa Kiwaaṱa wanapojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua makosa hayo. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiswa na Corder (1967) ndiyo iliyoongoza utafiti huu kwa kufuata misingi yake. Nadharia hii hutumiwa kuchanganua makosa katika matumizi ya lugha hasa vyanzo vya makosa hayo. Katika Nadharia ya Uchanganuzi Makosa, Corder anaeleza kuwa mtu yeyote aliyejifunza lugha ya pili hufanya makosa. Nayo nadharia hii inaweza kuyatambua, kuyaweka katika mafungu, kutambua chanzo chake na hata kuyarekebisha makosa hayo. Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji wa data ni mahojiano, uandishi wa insha na usomaji wa insha hizo. Mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano wakati wa kukusanya fonimu za lugha ya Kiwaaṱa. Vilevile, wanafunzi walipewa swali la insha, kisha wakaandika insha hizo na kabla ya kukusanywa, kila mwanafunzi alisoma insha yake kwa sauti huku mtafiti akirekodi usomaji huo na baadaye mtafiti alikusanya insha hizo akazisahihisha na kutambua na kuyachanganua makosa kwa kuongozwa na hatua zinazopendekezwa na Corder katika Nadharia ya Uchanganuzi Makosa. Utafiti huu ulihusisha shule tatu za upili katika sehemu ya Gede, Dabaso na Mijomboni ambapo katika kila shule, sampuli ya wanafunzi kumi iliteuliwa hivyo basi sampuli ya wanafunzi thelathini ndiyo iliyoteuliwa. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makosa mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wa Kiwaaṱa wanaojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili. Makosa hayo yalianishwa katika makundi matatu yafuatayo: Makosa ya matumizi ya sauti mbadala, makosa ya udondoshaji wa irabu na konsonanti na makosa ya uchopekaji wa konsonanti na irabu. vi Mtafiti alibaini kuwa makosa mengi yalitokana na tofauti za kimofofonolojia kati ya lugha ya kwanza ya wanafunzi hao ambayo ni Kiwaaṱa na lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya pili ya wanafunzi hao. Mtafiti vilevile alipendekeza mikakati ambayo ingetumiwa na walimu ili waweze kusaidia wanafunzi kuboresha matamshi na maandishi yao wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Mikakati iliyopendekezwa na mtafiti ni: kuorodhesha na kuwafundisha kwa kuwadhihirishia wanafunzi hao tofauti iliyopo kati ya fonimu za lugha hizi mbili. Vile vile mtafiti alipendekeza walimu kuchukua jukumu la kuwafanyisha mazoezi ya mara kwa mara ya kimatamshi na ya kimaandishi. Utafiti huu utakuwa na mchango wa kusaidia kuinua viwango vya elimu katika sehemu za Gede, Dabaso na Mijomboni. Vile vile utafiti huu utachangia pakubwa katika kuinakili na kuihifadhi lugha ya Kiwaaṱa katika kiwango cha isimu cha Fonolojia.Utafiti huu pia ni wa manufaa kwani utakuwa hazina kubwa katika usomi wa maktaba kwa sababu wasomi wataweza kurejelea kazi hii watakapokuwa wanashughulikia masuala kuhusu athari ya lugha ya kwanza katika lugha ya pili. Kuna tafiti chache ambazo zimefanywa kuhusu Waaṱa katika Mwambao huu wa Pwani, hivyo basi utafiti huu utaongeza ujuzi wa kiisimu kati
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/1036
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV