• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UDHANAISHI KATIKA RIWAYA ZA THOMAS KAMUGISHA: KITU KIDOGO TU! NA HARUSI YA WENDAWAZIMU

    Thumbnail
    View/Open
    ABDALLAH MZUNGU CHIMERAH.pdf (983.5Kb)
    Date
    2021-03-01
    Author
    CHIMERAH, ABDALLAH MZUNGU
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utafiti huu ulichunguza udhanaishi katika matendo na maneno ya wahusika katika riwaya mbili za Thomas A. R. Kamugisha; Kitu Kidogo Tu! na Harusi ya Wendawazimu. Hivyo, madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza matendo na maneno ya wahusika ili kudhihirisha vipengele vya kidhanaishi vinavyojitokeza. Utafiti huu umegawanywa katika sura tano; ya kwanza ni utangulizi yenye usuli wa mada, swala la utafiti, malengo ya utafiti, natija ya utafiti, upeo na mipaka ya utafiti na ufafanuzi wa istilahi na vifupisho. Sura ya pili imeeleza tafiti mbalimbali tangulizi za kuhusu udhanaishi na pia nadharia ya udhanaishi imefafanuliwa. Sura ya tatu imeeleza utaratibu wa utafiti, mbinu na vifaa vilivyotumiwa kukusanyia data na jinsi data hiyo ilivyochanganuliwa. Katika sura ya nne data iliyokusanywa imechanganuliwa. Sura ya tano imebeba muhtasari wa utafiti, hitimisho, mapendekezo kwa watafiti wengine na marejeleo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya udhanaishi inayohusishwa na wanafalsafa kama Soren Kierkegaard (1813-1855), Jean Paul Sartre (1905-1980), Friedrich Nietzsche (1844-1900). Udhanaishi ni falsafa inayoshugulikia maswala kuhusu maisha; ni mtazamo unaokagua kwa upembuzi hali ya nafasi ya mtu katika ulimwengu anamoishi. Mtafiti amegundua kuwa riwaya hizi mbili za Kamugisha ni za kidhanaishi kutokana na matendo na kauli za wahusika wake. Vipengele vya kidhanaishi kama utamaushi, ukengeushi, swala la uwepo wa Mungu, uhuru wa mtu binafsi na kuabudu mahitaji ya kimwili vimejitokeza. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kithamano na matokeo kuwasilishwa kwa maelezo ya kinathari. Utafiti ulikuwa wa maktabani.
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/1072
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV