• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    MOFOSINTAKSIA YA VITENZI VISABABISHI KATIKA LUGHA YA KIGIRYAMA

    Thumbnail
    View/Open
    EMANNUEL NYUNDO.pdf (715.2Kb)
    Date
    2023-10-11
    Author
    NYUNDO, EMMANUEL KAINGU
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utafiti huu ulihusu mofosintaksia ya vitenzi visababishi na ulichanganua jinsi mofimu mbali mbali zinavyoweza kugeuka katika uundaji wa vitenzi visababishi katika lugha ya Kigiryama. Hivyo basi, utafiti huu ulieleza mofosintaksia ya vitenzi visababishi vya lugha ya Kigiryama kwa kubainisha mofimu za vitenzi visababishi, kuchanganua miundo ya vitenzi visababishi na kubainisha utata katika baadhi ya vitenzi visababishi vya lugha ya Kigiryama. Nadharia ya Uminimalisti ambayo iliasisiwa na Chomsky (1957) ndiyo iliyotumika katika kuongoza utafiti huu wa vitenzi visababishi vya lugha ya Kigiryama. Nadharia hii ya uminimalisti hutilia mkazo uundaji wa sentensi ambazo huwa zinahitaji kuzingatia kanuni za upatanisho wa kisarufi na viambajengo vya maneno katika kategoria zote za kileksia. Nadharia ya Uminimalisti inaangalia miundo ya kirai kwa kuzingatia sheria za muainisho wa sauti na maana rejelewa katika lugha. Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji wa data ni matumizi ya hojaji na mazungumzo elekezi. Mtafiti alitumia mbinu ya hojaji na mazungumzo elekezi wakati wa kutafuta sentensi sahihi zilizoonyesha matumizi ya usababishaji katika lugha ya Kigiryama. Kila mzee kati ya wazee watano waliochaguliwa katika kila eneo la utafiti, alipewa sentensi thelathini. Sentensi hizo zilitakikana kuchanganuliwa na kutumia vitenzi ambavyo vilikuwa katika hali ya usababishaji. Sentensi hizo za wazee waliotumiwa kutoka maeneo mawili ya utafiti, ndizo zilizochukuliwa na kuunda data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha miundo tofauti tofauti ya jinsi mofimu hugeuka katika kuunda vitenzi visababishi katika lugha ya Kigiryama. Mofimu zilizojitokeza katika usababishaji zilikuwa zile za -ish, -esh, -iz, -ez na -vy. Pia, utafiti ulionyesha kwamba baadhi ya vitenzi visababishi katika lugha ya Kigiryama vinaonyesha utata katika matumizi yake. Miundo ya vitenzi visababishi katika lugha ya Kigiryama pia ilijitokeza na kuelezwa. Utafiti huu ulithibitisha kwamba kunazo aina tatu za usababishi katika lugha ya Kigiryama ambazo ni usababishi wa kileksia, kimofolojia na kisintaksia. Hata hivyo, japo utafiti ulishughulikia mofimu za vitenzi visababishi katika mofolojia na sintaksia, haukugusia mofimu za kileksia. Utafiti huu utakuwa na mchango wa kitaaluma katika isimu ya tafiti za Kigiryama na kichocheo cha tafiti zaidi za lugha ya Kigiryama. Vile vile, utafiti huu utachangia pakubwa katika kuihifadhi lugha ya Kigiryama katika kiwango cha Isimu cha mofosintaksia. Utafiti huu pia ni wa manufaa kwani utakuwa hazina kubwa katika usomi wa maktaba kwa sababu wasomi wataweza kurejelea kazi hii na kupata kichocheo cha matumizi zaidi ya Nadharia ya Uminimalisti. Kwa kuwa kuna tafiti chache za lugha ya Kigiryama ambazo zimefanywa kuhusu mada ya mofosintaksia na vitenzi vya usababishaji, utafiti huu utakuwa hazina muhimu ya siku za usoni katika maktaba za vyuoni.
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/1108
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV