Browsing Department of Linguistics, Languages and Literature by Issue Date
Now showing items 1-20 of 22
-
UCHANGANUZI WA MIUNDO YA VISHAZI KATIKA SENTENSI ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI
(Pwani Unversity, 2015-08-12)Kishazi ni kundi la maneno lenye uhusiano wa kiima- kiarifu hasa likiwa ndani ya sentensi kuu. Kikundi cha maneno hicho kinaundwa kwa elementi kadhaa, miongoni mwa elementi zake hizo lazima kiwemo kirai kitenzi. Kirai ... -
USAWIRI WA MWANAMUME KATIKA METHALI ZA KIMERU NCHINI KENYA
(Pwani University, 2016-08)Utafiti huu unahusu uchanganuzi wa usawiri wa mwanamume katika methali za Kimeru. Imebainika kuwa usawiri wa mwanamume katika methali za Kimeru haujawekwa bayana na utafiti wowote. Utafiti huu umebainisha jinsi ... -
MITAZAMO YA WAANDISHI WA KIKE NA WA KIUME KUHUSU USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIKE KATIKA TAMTHILIA ZA KISWAHILI
(Pwani University, 2017-10-12)Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza mitazamo ya waandishi wa kike na wa kiume kuhusu usawiri wa wahusika wa kike katika tamthilia za Kiswahili. Mtafiti aliongozwa na malengo matatu. Kwanza, ni kutambulisha ... -
NJEO, HALI NA DHAMIRA KATIKA KITENZI CHA KITIKUU: MTAZAMO WA UMINIMALISTI
(Pwani University, 2017-11-08)Tasnifu hii inahusu uchanganuzi wa kiufafanuzi wa kimofosintaksia wa njeo, hali na dhamira katika kitenzi cha Kitikuu. Njeo, hali na dhamira ni kategoria za kisarufi zinazopatikana katika kitenzi. Kitikuu ni lahaja ... -
UTENZI WA AL-INKISHAFI: DHIHIRISHO LA UHALISIAJABU KATIKA KUENDELEZA MAUDHUI YA DINI YA KIISLAMU
(Pwani University, 2018-05)Utafiti huu unahusu uchanganuzi wa kihalisiajabu kuendeleza maudhui ya dini katika Utenzi wa Al-Inkishafi wa Sayyid Abdallah bin Ali bin Nassir, mshairi mtajika aliyeishi katika kisiwa cha Pate baina ya 1718-1815 (Chiraghdin, ... -
UCHANGANUZI WA MAUDHUI YA NYIMBO ZA MSONDO NA ATHARI ZAKE KWA WANANDOA KATIKA JAMII YA WADIGO
(Pwani Unversity, 2018-05-15)Nyimbo za msondo za jamii ya Wadigo ni aina za nyimbo ambazo huimbwa wakati wa harusi upande wa kwa bi. harusi na huwa tofauti kabisa na nyimbo za harusi za kawaida. Utafiti huu ulinuia kuchanganua maudhui ya nyimbo za ... -
ATHARI ZA USASA KWENYE USIMULIZI WA HADITHI KATIKA JAMII YA WAMASAABA NCHINI UGANDA
(Pwani University, 2018-07-16)Kazi hii inahusu athari za usasa katika usimulizi wa hadithi miongoni mwa Wamasaaba nchini Uganda. Swala la utafiti ni kuwa mchango wa usasa katika usimulizi wa hadithi umezua maoni mbalimbali kutoka kwa wasomi tofautitofauti ... -
MAANA TIMILIFU KUTOKANA NA UNDIMI KATIKA UTENZI WA SIRI LI ASRARI
(Pwani Unversity, 2018-08-01)Utenzi wa Siri li Asrari ulitungwa katika karne ya 17 na mpaka sasa haujashughulikiwa ipasavyo. Ni utenzi unaozungumzia, kiubunifu, mojawapo ya vita vya Mtume Muhammad alivyopigana na wasioamini Uislamu. Mbali na hayo, ni ... -
UCHANGANUZI WA MAUDHUI YA SIASA KATIKA HADITHI MBILI, KIKAZA YA ROBERT ODUORI NA UTEUZI WA MOYONI YA RAYYA TIMAMMY
(Pwani University, 2018-10)Utafiti huu umeshughulikia uchanganuzi wa maudhui ya siasa jinsi yanavyodhihirika katika hadithi iliyotungwa na Oduori, Kikaza na hadithi iliyotungwa na Timammy, Uteuzi wa Moyoni. Mbali na kuchanganua maudhui, utafiti huu ... -
UHAKIKI WA MAUDHUI NA FANI KATIKA UTENZI WA MWANAMANGA UTUNZI WAKE FUMO LIYONGO
(Pwani University, 2018-10-01)IKISIRI Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa maudhui na fani katika Utenzi wa Mwanamanga. Utafiti huu ulilenga kuchunguza maudhui na vipengee vya fani vilivyodhihirika katika utenzi huo. Utafiti huu vilevile ulilenga kubainisha ... -
UCHANGANUZI WA ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA MIONGONI MWA WANAFUNZI WA KISOMALI WANAPOJIFUNZA LUGHA YA KISWAHILI
(Pwani University, 2019-07-28)Utafiti huu ulishughulikia makosa ya kimofofonolojia miongoni mwa wanafunzi wa Kisomali wanapojifunza Kiswahili sanifu kama lugha yao ya pili. Utafiti huu ulifanywa katika shule za upili za umma katika kaunti–ndogo ya ... -
UCHANGANUZI WA MAKOSA YA KIMOFOFONOLOJIA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI MIONGONI MWA WANAFUNZI WENYE ASILI YA LUGHA YA KIKAMBA
(Pwani University, 2020-05-04)Utafiti huu umechanganua makosa ya kimofofonolojia yanayofanywa na wanafunzi wa shule za upili ambao ni wazungumzaji wa lugha ya Kikamba wanapojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili. Utafiti huu ulinuia kutambua ... -
UDHANAISHI KATIKA RIWAYA ZA THOMAS KAMUGISHA: KITU KIDOGO TU! NA HARUSI YA WENDAWAZIMU
(ABDALLAH MZUNGU CHIMERAH, 2021-03-01)Utafiti huu ulichunguza udhanaishi katika matendo na maneno ya wahusika katika riwaya mbili za Thomas A. R. Kamugisha; Kitu Kidogo Tu! na Harusi ya Wendawazimu. Hivyo, madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza matendo ... -
USHAHIDI UNAODHIHIRISHA KUWA KISWAHILI SI KIARABU
(Pwani University, 2021-07-13)Utafiti huu umeonyesha kuwa Kiswahili ni lugha kamili, huru inayoweza kujisimamia kama lugha nyingine yoyote. Vilevile umepinga swala la kuwa Kiswahili ni Kiarabu. Maneno asili ya Kiarabu yamefanyiwa utafiti kwa njia ya ... -
UCHUNGUZI WA JINSI KUCHANGANYA NDIMI KATIKA MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI NA KIINGEREZA KUNAVYOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI SANIFU KATIKA CHUO KIKUU CHA PWANI
(Pwani University, 2022-03-03)Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi kuchanganya ndimi kunavyoathiri maendeleo ya lugha ya Kiswahili sanifu kutokana na maneno ya Kiingereza yanayochopekwa katika lugha ya Kiswahili wakati wa mawasiliano. Kuchanganya ndimi ... -
UCHANGANUZI WA MAKOSA YA KIMOFOFONOLOJIA YA WANAFUNZI WA KIWAAṰA WANAPOJIFUNZA LUGHA YA KISWAHILI
(Pwani University, 2022-03-14)Utafiti huu ulihusu uchanganuzi wa makosa ya kimofofonolojia ya wanafunzi wa Kiwaaṱa wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Hivyo basi utafiti huu ulilenga kueleza Fonolojia ya lugha ya Kiwaaṱa kwa kufafanua sifa ... -
STRUCTURAL ANALYSIS OF FAIRY TALES OF THE GIRIAMA OF RURAL KILIFI COUNTY IN KENYA.
(Pwani University, 2022-04-14)The study set out to carry out a structural analysis of Giriama fairy tales from the rural parts of Kilifi County in Kenya. This was informed by the structural analysis of tales that began with Propp’s ground-breaking ... -
MNYAMBULIKO WA VITENZI KATIKA LUGHA YA KIDIGO: MKABALA WA FONOLOJIA ZALISHI ASILIA
(Pwani University, 2022-04-21)Utafiti huu ulihusu mnyambuliko wa vitenzi katika lugha ya Kidigo kwa madhumuni ya kubainisha kanuni zinaohusika katika mchakato wa kunyambua vitenzi katika lugha hii. Kama lugha mojawapo ya Kibantu, lugha ya Kidigo ... -
THE MODERN AFRICAN WOMAN AS DEPICTED IN 'THE SMART MONEY WOMAN' A NOVEL BY ARESE UGWU.
(Pwani University, 2022-08-14)Incorporating a 21st century text by a female author whose work has not been studied in the literature terrain, this study sought to investigate and explore the depiction of the modern African woman as portrayed by Arese ... -
UCHANGANUZI WA TONOLOJIA YA KICHONYI KWA MKABALA WA NADHARIA YA FONOLOJIA VIPANDESAUTI HURU
(Pwani University, 2022-09-15)Toni katika lugha toni hudhihirika wakati wa uzungumzaji na hufanya neno kuwa na maana zaidi ya moja. Neno lenye toni linapotumika katika sentensi, mabadiliko ya toni huweza kuleta tofauti ya maana katika sentensi mahususi. ...