• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UHAKIKI WA MAUDHUI NA FANI KATIKA UTENZI WA MWANAMANGA UTUNZI WAKE FUMO LIYONGO

    Thumbnail
    View/Open
    HENRY MWALUGHA MWASAFU.pdf (640.8Kb)
    Date
    2018-10-01
    Author
    MWASAFU, HENRY MWALUGHA
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    IKISIRI Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa maudhui na fani katika Utenzi wa Mwanamanga. Utafiti huu ulilenga kuchunguza maudhui na vipengee vya fani vilivyodhihirika katika utenzi huo. Utafiti huu vilevile ulilenga kubainisha hisia ambazo mtunzi amezitumia katika utenzi huo kwa kuangazia tamathali mbalimbali za usemi zilizotumiwa kuibua hisia hizo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kihemenitiki iliyoasisiwa na Friedrich Schleiermacher, Wilhelm Dilthey na Martin Heidegger. Msingi wa mtazamo wa kihemenitiki ni uchunguzi wa matendo mbalimbali ya binadamu kama usemaji, upendaji na uchukiaji. Nadharia hii inalenga kuchunguza mawasiliano pamoja na ufasiri wa maana za matini mbalimbali kama vile: kazi za kifasihi, vifungu vya Bibilia na vya kifalsafa. Utafiti huu ni wa kimaelezo ambapo umehusisha usomaji wa maktabani na vilevile kuzuru nyanjani. Katika usomi wa maktabani, makala, vitabu pamwe na tasnifu mbalimbali za fasihi zilisomwa ili kupata data iliyohusiana na utafiti huu. Utafiti huu kwa kiwango fulani ulihusisha usakuraji na ukusanyaji wa makala faafu kupitia kwa mtandao katika tovuti mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Katika utafiti wa nyanjani, mtafiti alifanya uteuzi wa kimakusudi ili kupata sampuli ya walengwa alionuia kupata data kutoka kwao. Utenzi wa Mwanamanga umedhihirisha maudhui ambayo baadhi yanahusiana na wanawake kama vile: urembo, unyumba, sifa, nafasi ya mwanamke katika jamii nakadhalika. Utenzi wa Mwanamanga umesheheni vipengee vingi vya fani ambavyo baadhi yavyo ni: tamathali za usemi kama vile: sitiari au mafumbo, taswira, tashbihi, ukiushi katika ushairi na muundo. Mtunzi wa Utenzi wa Mwanamanga ametumia hisia kama vile: kuona, kuonja, kunusa, kugusa na kusikia katika kumwelezea mhusika wake kwenye utenzi.
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/710
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV