• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UTENZI WA AL-INKISHAFI: DHIHIRISHO LA UHALISIAJABU KATIKA KUENDELEZA MAUDHUI YA DINI YA KIISLAMU

    Thumbnail
    View/Open
    Ali Hamisi Chembea .pdf (1.002Mb)
    Date
    2018-05
    Author
    CHEMBEA, ALI HAMISI
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utafiti huu unahusu uchanganuzi wa kihalisiajabu kuendeleza maudhui ya dini katika Utenzi wa Al-Inkishafi wa Sayyid Abdallah bin Ali bin Nassir, mshairi mtajika aliyeishi katika kisiwa cha Pate baina ya 1718-1815 (Chiraghdin, 1987). Utenzi wa Al-Inkishafi ni mojawapo ya tungo tatu za kale maarufu sana Uswahilini hasa maeneo ya pwani Kaskazini. Utafiti huu umeangazia matumizi ya uhalisiajabu katika Utenzi wa Al-Inkishafi kuendeleza maudhui yanayoibua falsafa ya kidini kuhusu maisha ya binadamu. Vipengee vya kihalisiajabu katika kiwango cha wahusika na mandhari vimebainishwa na kuchanganuliwa katika mizani ya maisha ya jumuia ya Pate na mapisi yake ili kuendeleza maudhui ya dini. Uajabu wa wahusika na mandhari ulikuwa kichocheo msingi kwa mtafiti kuamua kushughulikia mada hii. Uchanganuzi huu uliongozwa na nadharia ya uhalisiajabu iliyoasisiwa na Franz Roh mwaka wa 1925 ambayo inayatazama matukio katika maisha ya binadamu kwa upeo ulio juu ya uhalisia kama ulivyozoeleka au kufahamika na binadamu; huangazia ulimwengu wa kidhahania sio ukweli kama ulivyo katika mazingira. Uteuzi wa sampuli ni Utenzi wa Al-Inkishafi wa Sayyid Abdallah bin Ali bin Nassir. Malengo ya utafiti huu yamekuwa: kubainisha wahusika na mandhari yanayodhihirisha uhalisiajabu, kueleza namna wahusika na mandhari ya uhalisiajabu yanavyoendeleza maudhui na kubainisha athari za maudhui ya dini kwa waumini zinazosawiriwa katika Utenzi wa Al-Inkishafi. Data ya kimsingi ilikusanywa maktabani kwa kusoma kazi teule, vitabu, majarida, tasnifu na katika mtandao. Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia teule. Aidha, mifano iliyotumika imetoka katika Utenzi wa Al-Inkishafi kulingana na ufanifu wake. Utafiti huu umeweka bayana kwamba uhalisiajabu kama mkabala wa kifasihi unadhihirika katika Utenzi wa Al-Inkishafi (1810-1820) kuendeleza vi maudhui ya dini japo uliasisiwa mwaka wa 1925 zaidi ya miaka mia mbili baada ya kutungwa utenzi huu.
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/711
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV