ATHARI ZA USASA KWENYE USIMULIZI WA HADITHI KATIKA JAMII YA WAMASAABA NCHINI UGANDA
Abstract
Kazi hii inahusu athari za usasa katika usimulizi wa hadithi miongoni mwa Wamasaaba nchini Uganda. Swala la utafiti ni kuwa mchango wa usasa katika usimulizi wa hadithi umezua maoni mbalimbali kutoka kwa wasomi tofautitofauti yanayokinzana. Baadhi ya wasomi hao wanaona kuwa usasa umechangia pakubwa sana uimarikaji wa hadithi katika jamii na wengine wanaona kuwa usasa ndio umechangia ufifiaji wa hadithi katika jamii mbalimbali. Kwa hiyo, utafiti huu ulidhamiria kuziba pengo ambalo linasababishwa na maelezo kinzani ya wasomi tofautitofauti kuhusu mchango wa usasa katika usimulizi wa hadithi. Madhumuni katika utafiti huu yalikuwa: Kubainisha mambo ya kisasa ambayo yameshuhudiwa katika jamii mbalimbali kuanzia karne ya 20, kueleza athari za mambo hayo katika usimulizi wa hadithi na kueleza mustakabali wa utamaduni wa kusimulia hadithi katika jamii ya Wamasaaba.
Katika kazi hii, mtafiti aliongozwa na nadharia ya usasashaji. Nadharia hii iliasisiwa na Marx (1864). Kwa mujibu wa Marx (1864), nadharia hii hutumiwa kueleza mchakato wa mabadiliko katika jamii kutokana na usasa. Mkabala wa utafiti katika kazi hii ulikuwa wa nyanjani. Mtafiti alitumia mkabala huu kwa sababu ulikuwa njia ya pekee ambayo ingemleta pamoja na wazee wenye maarifa ambayo wangempa maneno ya busara. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaendeleza mahojiano na wahojiwa pamoja na kusambaza hojaji. Mahojiano yaliyoendelezwa yalimwezesha mtafiti kukusanya taarifa mbalimbali kuhusu hadithi miongoni mwa Wamasaaba. Taarifa zilizokusanywa zilijumulisha maelezo kuhusu mambo ya kisasa ambayo yameshuhudiwa katika jamii ya Wamasaaba kuanzia karne ya 20 hadi sasa, athari zake katika usimulizi wa hadithi na mustakabali wa utamaduni wa kusimulia hadithi katika jamii hiyo. Kwa jumla