• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    UCHANGANUZI WA MIUNDO YA VISHAZI KATIKA SENTENSI ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI

    Thumbnail
    View/Open
    AMINA COVER PAGES UTAFITI AMINA YA KUWASILISHA.pdf (177.0Kb)
    amina UTAFITI AMINA 22.pdf (707.2Kb)
    Date
    2015-08-12
    Author
    Khamis, Amina Ali
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Kishazi ni kundi la maneno lenye uhusiano wa kiima- kiarifu hasa likiwa ndani ya sentensi kuu. Kikundi cha maneno hicho kinaundwa kwa elementi kadhaa, miongoni mwa elementi zake hizo lazima kiwemo kirai kitenzi. Kirai kitenzi ndicho kinachounganisha kati ya mtenda na kitendwa au mtendwa katika sentensi. Jambo hili pia limeonekana katika sentensi za lahaja ya Kimakunduchi, kwani kuna miundo na sheria zinazotawala kuundia vishazi na viaina vya vishazi alivyovibaini mtafiti katika utafiti huu. Hivyo, utafiti huu umevielezea kwa kina vishazi hivyo na viaina vyake. Tafiti nyingi za waandishi tofauti wamejaribu kuelezea dhana ya kishazi na aina zake kuwa kuna kishazi tegemezi na kishazi huru kwa kuangazia lugha ya Kiingereza na Kiswahili sanifu. Hakuna mtafiti yeyote aliyefanya utafiti kwa lahaja ya Kimakunduchi uliochambua na kubainisha miundo na sheria zake za kisarufi za kuundia vishazi na viaina vya vishazi hivyo. Hili ndilo tatizo alilolichunguza mtafiti katika utafiti huu. Madhumuni ya utafiti huu ni kutambulisha aina ya vishazi vya lahaja ya Kimakunduchi. Kubainisha miundo ya vishazi ndani ya sentensi za lahaja ya Kimakunduchi pia kubainisha sheria zinazotawala kuundia vishazi hivyo ndani ya sentensi za lahaja ya Kimakunduchi. Nadharia ya uminimalisti iliyoasisiwa na Chomsky ndio muongozo wa utafiti huu. Chomsky anaamini msingi mkuu wa nadharia hii ni umilisi na utendaji na mihimili ya nadharia hii ni umbo fonetiki na umbo mantiki. Data ya msingi ya utafiti huu ni sentensi zilizotolewa kutokana na masimulizi ya wazawa wa lahaja hii ya Kimakunduchi, waliopatikana kutoka shehia tano za kijiji cha Makunduchi, ambako ndiko wanakoishi wazawa hao. Data iliyokusanywa ilibainika kuwa kuna aina kuu mbili za vishazi ambazo kila moja ilibaniwa kuna viaina vitatu ndani yake. Kishazi huru kilitowa kishazi huru tamko, kishazi huru agizi na kishazi huru suali. Kishazi tegemezi kilitowa kishazi tegemezi rejeshi, kishazi tegemezi shuruti na kishazi tegemezi kiunganishi . Aina zote hizo za vishazi zimetupatia miundo katika vishazi huru na miundo katika vishazi tegemezi. vi Utafiti huu utaleta manufaa kwa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji wa lahaja hususan ya Kimakunduchi, pia kwa wanafunzi na walimu wa sarufi na lugha. Hii ni kwa sababu wanafunzi wengi hupendelea kujifunza lahaja kwa kutaka kupata kuelewa miundo na sheria zinazotawala kuundia miundo hiyo. Pia utafiti huu utakua changa moto kwa watafiti wangine kuangazia kishazi katika lahaja nyengine pia kubaini pengo la kitaaluma katika lahaja hii ya Kimakunduchi
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/792
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV