• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    •   Repository Home
    • Electronic Theses and Dissertations
    • Masters Theses and Dissertations
    • Department of Linguistics, Languages and Literature
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    MAANA TIMILIFU KUTOKANA NA UNDIMI KATIKA UTENZI WA SIRI LI ASRARI

    Thumbnail
    View/Open
    MOHAMED RAMADHAN KARAMA.pdf (8.763Mb)
    Date
    2018-08-01
    Author
    KARAMA, MOHAMED RAMADHAN
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utenzi wa Siri li Asrari ulitungwa katika karne ya 17 na mpaka sasa haujashughulikiwa ipasavyo. Ni utenzi unaozungumzia, kiubunifu, mojawapo ya vita vya Mtume Muhammad alivyopigana na wasioamini Uislamu. Mbali na hayo, ni utenzi unaokazania waumini kumuomba Mungu katika matatizo yao kupitia majina Yake matukufu. Mwitifaki mkuu wa nadharia ya Usemezano, Mwanaisimu Mikhail Bakhtin, haoni kama ushairi una usemezano au undimi, hali ya kuwa na aina za lugha katika uwasilishaji wake. Kimtazamo wake lugha ya kishairi ni ya uzungumzi nafsia, imefungika, haibadiliki na haikubali aina nyingine za lugha kujumuika ndani yake. Zaidi, inafanana na lugha ya kidini ambayo ni ya kiimla, kitaasubi na haikosoleki au kupingwa. Utafiti huu ulijikita kugeuza msimamo huu wa lugha ya kishairi pamoja na lugha ya kidini katika kutoa maana. Ili kufikia lengo letu tulitumia madhumuni matatu: kuufafanua utenzi huu katika muktadha wa kisufi; kubainisha ufungamanisho wa ainati za lugha zilizomo ndani ya utenzi; na kujadili lugha ya kidini kuwa kipengele cha undimi. Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa kuzingatia msamiati, mbinu za uwasilishaji wa msamiati huo, masimulizi yaliyomo ndani ya utenzi, na maingiliano ya aina hizi za lugha. Kimsingi, utafiti wetu ulikuwa wa kimaelezo ya matini ya utenzi huu. Hata hivyo, mahojiano yalifanywa kwa kuchagua sampuli stahiki ambayo ilikuwa na uzoefu mkubwa wa kilugha na kiutaalamu kuhusu maswala ya kishairi, kidini na kitamaduni yaliyotajwa katika utenzi huu. Uchanganuzi wetu ulitudhihirishia ainati za lugha za kitaalamu, kishajara, kimahsusi, kifasihi, kikawaida, na kidini. Ainati hizo za lugha zinaweka wazi maana za maneno katika uwasilishwaji wake katika muktadha wa kilugha na kitamaduni. Tunahitimisha kwamba ushairi unazo sifa za matumizi ya ainati ya lugha na pia lugha ya kidini, aliyoipinga Bakhtin, ina jukumu katika kufikiliza ujumbe na maana timilifu kupatikana. Kwetu sisi ufafanuzi wa utenzi huu una natija si kwa wasomaji wa mashairi na fasihi yote ya Kiswahili kwa jumla bali pia umeishajiisha nadharia ya Usemezano kwa kuangaziwa ushairi na lugha ya kidini.
    URI
    http://elibrary.pu.ac.ke/handle/123456789/805
    Collections
    • Department of Linguistics, Languages and Literature

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of PUSpaceCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2016  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    Atmire NV